2 Kings 25:27-30

Yehoyakini Anaachiwa

(Yeremia 52:31-34)

27 aKatika mwaka wa thelathini na saba tangu Yehoyakini mfalme wa Yuda apelekwe uhamishoni, katika mwaka ule ambao Evil-Merodaki
Pia aliitwa Ameli-Mariduki.
alifanyika mfalme wa Babeli, alimwacha huru Yehoyakini kutoka gerezani siku ya ishirini na saba ya mwezi wa kumi na mbili.
28 cAlizungumza naye kwa upole na kumpa kiti cha heshima zaidi kuliko wale wafalme wengine aliokuwa nao huko Babeli. 29 dHivyo Yehoyakini akayavua mavazi yake ya mfungwa, na siku zote za maisha yake zilizobaki alikula mezani mwa mfalme. 30 eSiku kwa siku mfalme alimpa Yehoyakini posho siku zote za maisha yake.

Copyright information for SwhNEN